Saturday 18 April 2015

Jinsi ya kutengeneza kucha zako

















































Kucha zinaweza kuchangia kwa kiasi kikubwa kuboresha mwonekano wako kama utazijali kuzipenda na kuzitunza vizuri.

Ni jambo la busara na linalopendeza kama ukijitahidi kuweka kucha zako katika hali ya
 usafi kwa kuziosha vizuri na kuzikata katika saizi ya kupendeza.

Kuna baadhi ya watu wanaopenda kufuga kucha zao japo sio salama sana kiafya. Ila kama umependa kufuga kucha zako basi jitahidi kuzifanyia usafi wa hali ya juu ili ziwe na mwonekano wa kuvutia na kupendeza zaidi.

Kucha nzuri na zenye matunzo zinaongeza urembo wako kwa wanawake pia  kwa wanaume zinakufanya uvutie zaidi na kuonekana wa kisasa.


Pia kucha zinaweza kuongeza mvuto zaidi pale zinapopakwa rangi kwa mpangilio mzuri na unaofaa.

Friday 3 April 2015

Dressing table













Ni aina ya meza iliyotengenezwa kwa staili ya kuvutia yenye kioo na ni maalumu kwaajili ya kujiweka sawa na kujiangalia wakati wa uvaaji wako, na urembo kwa ujumla yani kujifanyia make up.

Meza hii ni maalumu kwaajili ya watu wote na jinsia zote, wanaume na wanawake.

Kwa kawaida kila binadamu anayejitambua na hasa vijana ni lazima awe na dressing table yaani sehemu kwa ajili ya kuwekea vipodozi vya mwili wake kama mafuta, chanuo, poda,wanja, lipstick nk.

Si vyema kuchanganya vipodozi na vitu vingine kwani kibinadamu sio ustaarabu,  ndiyo maana basi ikatengwa sehemu maalumu kwaajili ya vitu vyako kama ivyo.

Aina hii ya meza ipo katika muundo tofautitofauti nay a kupendeza sana.