Thursday 26 March 2015

jinsi unavyoweza kutengeneza nyusi zako



 


 Unaweza kutengeneza nyusi zako na kuzifanya zionekane katika mwonekano wa kupendeza zaidi.kwa  kuzichonga  katika mpangilio unaofaa na kuzipaka wanja ili kuwa   katika mwonekano wa kuvutia zaidi.

Nyusi huongeza mvuto hasa kwa mwanamke pale zinapokuwa zinatengenezwa mara kwa mara na kuwekwa katika mpangilio unaofaa.

Kuna aina mbalimbali za upakaji wanja hii inategemea ni jinsi gani umezichonga nyusi zako. Unaweza kupaka ukianzia kwa upana kwenda wembamba au wembamba kote au nene kote inategemea pia na jinsi unavyopendelea

Suala la utengenezaji nyusi ni bora kuzingatiwa kwa kuwa linaongeza mvuto kwa wanawake

Tuesday 24 March 2015

makeup








 







·         the way in which something is put together or arranged
·         the physical, mental, and moral character of a person
·         substances (such as lipstick or powder) used to make someone's face look more attractive

 Kujifanyia makeup ni hali ya kujiweka katika muonekano wa kuvutia zaidi. 

Watu wengi wamekuwa wakionekana tofauti na wenye mvuto wa hali ya juu  hii ni kutokana na mpangilio mzuri wa makeup katika nyuso zao kwa kutumia lipstick za aina mbalimbali powder zinazoendana kabisa na rangi ya nguo wanazovaa.

Utaonekana vizuri zaidi pale utakapotumia make up inayoendana na rangi yako ya mwili. Kwani kuna make up anayoweza kutumia mtu wa rangi nyeupe rangi ya chocolate na mweusi kabisa, hizi zinatofautiana   na rangi zake. 

Ni vyema basi kuchagua makeup inayoendana na rangi ya ngozi yako ili uonekane wa kuvutia zaidi.
























Monday 16 March 2015

Boresha mwonekano wako kwa kuvaa cheni






Kuwa maridadi  ni sifa ya kila binadamu aliye kamilika,  anayejipenda na kuijua dhamani ya mwili wake. Ila pia unaweza kuongeza mvuto wa mwonekano wako na kuonekana maridadi zaidi  kwa kuvalia cheni katika shingo yako.

 Hii husaidia pia shingo kukaa vizuri na kujisikia umaridadadi zaidi.

Kila mtu huwa na aina tofauti tofauti ya cheni anayopendelea, hii inatokana na jinsi ya mpangilio wako wa uvaaji kwani kuna wengine hupendelea cheni kubwa, wengine saizi ya kawaida na wengine ndogo kabisa.

Ni vizuri kuzoesha shingo yako kuvaa cheni kwani  inakufanya uonekane  maridadi na nadhifu zaidi